Jumatatu, 29 Juni 2015

Vitate, Vitawe na Visawe

Vitate, Vitawe na Visawe
..........................................................................................................................................
Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni:

  1. Vitale : maneno yanayotatiza kimatamshi.  Vitate hutatiza kimatamshi
  2.  Vitawe: maneno yenye maana zaidi ya moja.  Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi
  3. Visawe: maneno tofauti yenye maana sawa  => Visawe huwa na maanasawa
.........................................................................................................................................
Vitate:
.........................................................................................................................................
Maneno yanayotatiza kimatamshi.
ndoa na doa :
ndoa 
kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke
doa  alama ya uchafu, kasoro au dosari
baba na papa :
baba 
mzazi wa kiume
papa  mnyama wa baharini
fua na vua :
fua 
osha nguo, tengeneza vyuma
vua  shika samaki kutoka majini; toa nguo
faa na vaa :
faa 
inayostahili, inayopaswa
vaa  weka nguo juu ya mwili
ngoma na goma :
ngoma 
ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa
goma  acha kufanya kazi
shinda na shida :
shinda 
ongoza katika makabiliano, mashindano
shida  taabu au matatizo
...................................................................................................................................
Vitawe :
...................................................................................................................................
Mano yenye maana zaidi ya moja
PAA :
kwea (enda juu), mnyama wa porini anayefanana na mbuzi au sehemu ya juu ya nyumba
SHINDA :
kaa au ishi mahali/wakati Fulani, ongoza katika shindano  au tupu
KAA :
sehemu yenye moto ya kuni, mnyama wa majini , keti chini au kuwa mahali fulani kwa muda
MBUZI :
mnyama anayefugwa kama ng'ombe au chombo cha kukunia nazi
MLANGO :
ukoo au watu wenye asili smoja, sehemu ya kuingia kwenye nyumba au kitu kinachotumika kifunga nyumba
FUA :
unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma au osha nguo
....................................................................................................................................
Visawe
....................................................................................................................................
Maneno tofauti yenye maana sawa.
msichana au banati : kijana wa jinsia ya kike
mvulana au ghulamu : kijana wa jinsia ya kiume
huzuni au majonzi : hali ya kilio na huruma
mazishi au matanga : shughuli za kumzika marehemu
wakati au mwia : wakati au muda
mtu au mja : mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki
barua au waraka : kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani
siri au faragha : jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine
macho au maninga : sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona
mwangaza au nuru : miyale inayowezesha watu kuona vitu
Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : Majina ya Mwenyezi Mungu
.........................................................................................................................................

Maoni 1 :