Ijumaa, 23 Oktoba 2015

NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE

Kumpa mtu ukweli wake                  =>  Kumwambia mtu wazi [to be transparent]
Pua kukaribiana kushikana na uso     =>  Kukunja uso kwa hasira [to express anger]
Sina hali                                            => Sijiwezi  [I am helpless (mostly when talking about love)]
Kupiga uvivu                                     => Kukaa tu bila kazi [abject laziness]
Kupiga kubwa                                   =>  Kwenda moja kwa moja [vanishing act]
Kumwekea mtu deko                         =>   Kulipiza  kisasi [pay back]
Mtu mwenye ndimi mbili                     =>  Kigeugeu  [A turncoat]
Miamba ya mitishamba                       => Wanga hodari wa kienyeji [ expert wizardry]
Kupiga supu                                       => Tegea  [do the least]
Kupiga mali shoka                              => Gawana  [distribute (contraband, bullion, inheritance]
Amekula chumvi nyingi          =>Ameishi miaka mingi [lived a long life]
Ahadi ni deni                          =>Timiza ahadi yako [be trustworthy; keep your promise]
Amewachukua wazee wake    => Anawatunza vizuri wazazi wake [taking good care of parents]
Amekuwa popo                      -=>Yu kigeugeu [ a turncoat]
Amevaa miwani                      =>Amelewa pombe [chakari] [inebriation, a drunkard]

Kuchungulia  kaburi                 =>Kunusurika kifo   [saved from a worse fate]
Fyata mkia                              => Nyamaza [keep silent]
Fimbo zimemwota mgongoni    =>Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni [birching scars on                                                         ones' back]
Hamadi kibindoni                    =>Akiba iliyopo kibindoni [savings for a rainy day]
Hawapikiki chungu kimoja       =>Hawapatani kamwe !  [always at loggerheads]
Kupika majungu                      => Kufanya mkutano wa siri [conspire a secret meeting]
Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka   =>  Kumsifu mtu kwa unafiki [kinafiki] [paying lip service]
Kula mlungula                          => Kula rushwa [receiving a bribe]
Kupelekwa miyomboni            => Kutiwa [kupelekwa] jandoni [performing circumcision]
Kujipalia mkaa                         => Kujitia matatani [get yourself in trouble]
Amekuwa mwalimu                => Yu msemaji sana  [a talkative person]
Amemwaga unga                     => Amefukuzwa kazi [ dismissed from employment]
Ana ulimu wa upanga               =>Ana maneno makali  [biting words]
Ameongezwa unga                  => Amepandishwa cheo [promoted]
Agizia risasi                             =>Piga risasi  [shoot!]
Chemsha bongo                      => Fikiri kwa makini  [think analytically]
Kumeza [zea] mate                  => Kutamani   [to crave for]
Kumuuma mtu sikio                 => Kumnong'oneza mtu jambo la siri [tell a secret to someone]
Kumpa nyama ya ulimi             =>Kumdanganya mtu kwa maneno matamu [using wiles to tell lies]
Kumchimba mtu                      => Kumpeleleza mtu siri yake  to dig one's secrets]
Kutia chumvi  katika mazungumzo  =>  Kuongea habari za uwongo [tell lies]
Vunjika moyo                          =>  Kata tamaa [give up]
Utawala msonga                               => Utawala wa wachache [leadership of the few]
Usiwe nyang'au                                 => Usidhulumu kwa kutumia madaraka
                                                                [Don't use your position to exploit others]
usiwe Kikaragosi                              =>  Usiwe chui katika ngozi ya kondoo
                                                                [Don't be a sheep in a leopard's skin]
Umangimeza                                     =>  Viongozi wanaopenda kuamrisha watu [a Dictatorship]
Kutoa ya mwaka                               => Kufanya jambo zuri na la pekee [performing a unique act]
Kula vumbi                                         => Pata taabu   [struggle]
Mafungulia ng'ombe                            => Kati ya saa mbili na saa tatu
                                                                   [between 8.00  and 9.00 o'clock
Kutia kiraka                                        => Fichia siri [confiante]
Kumlainisha mtu                                  -=> Kumzungumzia mtu maneno

Yalimkata maini                       - Yalimtia uchungu  [emotional pain]
Kujikosoa                               => Kujisahihisha  [correct your ways]
Kutia utambi                            => Kuchochea ugomvi  [convince someone to fight]
Kumeza maneno                      => Kutunza siri moyoni  [to keep a secret]
Kula njama                              => Kufanya mkutano wa siri [to conspire a secret meeting]
Kumkalia mtu kitako                => Kumsema/kumsengenya  [to talk about someone]
Kupiga vijembe                        => Kumsema mtu kwa fumbo [use idioms to talk about someone]
Kiinua mgongo                         => Malipo ya pongezi/uzeeni [pension]
Kazi ya majungu                       => Kazi ya kumpatia mtu posho [hand to mouth existence]
Kaza kamba                             => Usikate tamaa - [never give up!]
Kumwonyesha mgongo             =>  Kujificha - [to hide]
Kuona cha mtema kuni             =>  Kupata mateso [torture]
Maneno ya uwani                     => Maneno yasiyo na maana/porojo  -  [hyperbole !]
Mate ya fisi                              =>  Kata tamaa kupita kiasi - [give up totally !]
Mbiu ya Mgambo                     => Tangazo [advertisement]
Mungu amemnyooshea kidole   => Mungu amemuadhibu -  [God's punishment]
Mkubwa jalala                          => Kila  lawama hupitia kwa mkubwa -
                                                       [The eldest is the Dumping ground!]
Mkaa jikoni                               => Mvivu wa kutembea -  [a stay at home person]
Mungu si Athumani                    -=>Mungu hapendelei [God is fair]
Ndege mbaya                            => Bahati mbaya [bad luck]
Paka mafuta kwa mgongo wa chupa => Danganya [telling lies]
 Usiwe kabaila                                  => Usichume tokana na jasho la mwingine [Don't exploit others]
Usiwe kupe                                      =>  Fanya kazi [be gainfully employed]
Usiwe bwanyenye                             =>  Usichume kwa vitega uchumi vyako [don't be a capitalist!]
Usiwe na mrija                                  =>  Usinyonye wenzako  [don't be exploitative]

Maoni 223 :

  1. Amepiga maji
    Ameuchapa mtindi

    JibuFuta
  2. Nini maana ya kula mwata?

    JibuFuta
  3. Watu wana kokotana
    Kwenda joshi

    JibuFuta
  4. mtoto kikopo nini maana yake?

    JibuFuta
  5. Kazi nzuri, songa mbele. Ongezea"amepata naizesheni" _ pata kazi/pandishwa cheo

    JibuFuta
  6. Nini maana ya nahau " Pangu pakavu, tia mchuzi"

    JibuFuta
    Majibu
    1. Watu wenye maisha magumu... Au watu masikini

      Futa
    2. kuomba msaada, nikama vile mnakula wali wali alafu upande wako unaona hauna mchuzi hutopata ladha vizuri.... kwahiyo unaomba mchuzi kidogo

      Futa
  7. nini maana ya nahau mtoto wa kikopo

    JibuFuta
  8. Alaye yu ala ala aliwa
    Naomba maana yake

    JibuFuta
  9. Maana ya watu wa chochole

    JibuFuta
  10. Nini maana ya kukata kitanzi

    JibuFuta
  11. Nini maana ya nahau,"kula mumbi".

    JibuFuta
  12. Nini maana ya nahau,"kula mumbi".

    JibuFuta
  13. Nini maana ya nahau,"tia kidala cha mdomo ".

    JibuFuta
  14. Nini maana ya nahau,"tia kidala cha mdomo ".

    JibuFuta
  15. Majibu hakuna kwa hiyo sioni kama i atusaidia

    JibuFuta
  16. Nini maana ya kazi za kijungu jiko

    JibuFuta
  17. Kazi ya kijungu jiko ni ile kazi inayokupatia fedha kwa ajili ya chakula tu, fedha kidogo kiasi kwamba huwezi kujiwekea akiba.

    JibuFuta
  18. Kuna nahau za zamani zinazojulikana sana Kama vile
    Ana mkono was birika
    Ana mkono mrefu
    Amepata jiko
    Amekuwa kichwa na nyinginezo

    JibuFuta
    Majibu
    1. Ana mkono wa birika ni mchoyo
      Ana mkono mrefu ni mwizi

      Futa
  19. maana ya kula mumbi tafadhali.

    JibuFuta
  20. (gipalia mkaa) jibu ya hilo nahau?

    JibuFuta
  21. majibu ya hizi nahau
    01-kula kwa macho?
    02-kujikaza kisabuni
    03-kufa kiume
    04-kavaa shati la mikono mirefu
    05-Tia chumvi
    06-Babu katundika wana
    07-kuwa popo

    JibuFuta
  22. Maana ya nahau "kufa kiofisa"

    JibuFuta
  23. Kazi nzuri. Mini maana ya ota mizizi

    JibuFuta
  24. 2.kuvumilia maka mwisho
    3.kishujaa
    4.kutoa rushwa
    5. Ongeza maneno ya uongo
    7.kigeugeu

    JibuFuta
  25. kufa kondoo maana yake ni ipi?
    Kinywa maji maana yake nini? Na
    Fata mkia pia ina maana gani? Wanagenzi tusaidiane

    JibuFuta
  26. Nini maana ya kumpa utokole

    JibuFuta
  27. Maana ya nahau amekuwa kibunye

    JibuFuta
  28. Kupiga kibiriz maana yake nini

    JibuFuta
  29. Nahau'kufa kiume' mini maana yake

    JibuFuta
    Majibu
    1. kuvumilia maumivu na mateso yanayokukumba

      Futa
  30. Maana ya kupata naizesheni ni?

    JibuFuta
  31. Nini maana ya nahau kuonja uso

    JibuFuta
  32. maana ya nahan hii, piga winda

    JibuFuta
  33. Maana y 'kula vya mwiki'

    JibuFuta
  34. Ilikua karibu akamatwe na simba maana take nin jaman

    JibuFuta
  35. maana ya ;tia mrija,kumpiga mtu sifa azizozistahili,kuwa na nafua

    JibuFuta
  36. Mini maana ya nahau pigs chuku

    JibuFuta
  37. Mini maana ya nahau piga chuku

    JibuFuta
  38. Nini maana ya nahau
    Kunoa lubu"
    Kulamba mtu kisogo"

    JibuFuta
  39. ni nini maana ya kata shauri

    JibuFuta
  40. Nini maana ya neno kupiga teke

    JibuFuta
  41. Maana ya zunguka mbuyu
    Piga mbiu
    Piga chenga
    Kwenda hana
    Toa rushwa

    JibuFuta
  42. Nini maana ya nahau piga winds?

    JibuFuta
  43. Maana ya nahau shika hatamu ni?

    JibuFuta
  44. Nahau yenye maana sawa na tungo zifuatazo
    1;Jumanne ni kijana mchoyo
    2;Yule ni mlopokaji Sana

    JibuFuta
  45. Nini maana ya nahau kufa kiofisa??

    JibuFuta
  46. Maana ya pata ashekali

    JibuFuta
  47. Maana ya ana miguu ya bata

    JibuFuta
  48. Maana ya kulamba kisogo ni ipii

    JibuFuta
  49. Moyo wa bua Ni moyo usiohimili vishindo

    JibuFuta
  50. Nini maana ya kupiga chuku

    JibuFuta
  51. Nini maana ya kuvaa koti la mtu

    JibuFuta
  52. Nini maana ya piga ukope?

    JibuFuta
  53. Piga maji ,,maana yake tafadhari nisaidieni

    JibuFuta
  54. Maana ya nahau Kaba roho

    JibuFuta
  55. Maana ya fanya fii?
    Piga kijembe?

    JibuFuta
  56. Ni semi gani Ina maana ya kuondolewa madaraka

    JibuFuta
  57. Tilia mrija inamaanisha...

    JibuFuta
  58. "Fuata nyayo" maana take ni Nini?

    JibuFuta
  59. Nini maana ya nahau " kutafuna maneno"?

    JibuFuta
  60. Ni nini maana ya pata ubeleko?

    JibuFuta
  61. nahau nyingi hazna mjb jamn

    JibuFuta
  62. Anua malago je maana yake nini?

    JibuFuta
  63. Nini maana ya nahau "kufa
    kiofisa"?

    JibuFuta
  64. Maana ya nahau shika hatamu

    JibuFuta