Jumanne, 6 Oktoba 2015

METHALI ZA KIUTANDAWAZI(GLOBAL -PROVERBS)

1.Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo
Kutokana na tabia ya kibinadamu, mtu hutambulika kwa uungwana wake kwa vitendo vyake wala siyo kwa mavazi, maumbile au maneno ayasemay

Public opinion maintains, a gentleman is judged by his actions. (Manners make man; or Handsome is as handsome does).

2. Akili ni nywele kila mtu ana zake
Akili za watu ni za aina nyingi na ni tofauti kama vile nywele za kila binadamu ni tofauti.  

Brains are like hair, every humankind has her/his own kind.

3.Baada ya dhiki faraja
Baada ya shida huja raha.

After hardship comes relief. (Every cloud has a silver lining; After storm comes a calm).

4.Bandubandu huisha (humaliza) gogo
Hata gogo liwe kubwa namna gain, unapolichanachana mwisho gogo hilo humalizika.

Chip! Chip! Finishes the log. (Little strikes fell great oak. Constant dripping wears away a stone).

5.Chanda chema hufikwa (huvishwa) pete
Jambo jema husifiwa na hushangiliwa ili liweze kufana zaidi. Ni wana kama kidole kizuri kinapovalishwa pete ili kizidi kupendeza.

A handsome finger gets a ring put round it.

6.Chema chajiuza kibaya chajitembeza
Kitu kizuri huonekana bila ya kunadiwa, lakini kibaya hupigiwa debe ili kukitangaza.

A good thing sells itself, a bad thing advertises itself for sale. (Good wine needs no bush). 

7.Dalili ya mvua ni mawingu
Ishara ya kuwa mvua itanyesha hivi punde ni mawingu meusi makubwa. Na yasipokuwepo mawingu haiwezi kunyesha. Hali kadhalika, katika juhudi zako waweza kujua mapema kama utafanikiwa
.
Clouds are the sign of rain. (Morning shows the day as the childhood shows the man. Cunning events cast their shadows before. No smoke without fire).
  
8.Damu ni nzito kuliko maji
Watu wa ukoo mmoja husaidiana sana katika matatizo yao kuliko marafiki au jamaa wa mbali.

Blood is thicker than water.

9.Elimu haina mwisho
Elimu ni za aina nyingi. Kila siku maarifa ya aina mpya yanagunduliwa na kuzuka, hivyo haiwezekani kuielewa elimu yote duniani.

Education has no limits. (One has to continue to learn all his/her life time).
  
10.Elimu ni bahari
Elimu ni pana hivi sawa na upeo wa bahari ambayo huelezwa na kusambazwa miongoni mwa binadamu. 

Education is like an ocean which spread all over the horizons of people’s life.

11.Fadhili za punda ni mashuzi
Shukrani za mtu mjinga ni kumtukana yule aliyemtendea mema.

The gratitude of a donkey is a breaking of wind.

12.Fimbo ya mbali haiuwi nyoka
Fimbo iliyo karibu nawe ndiyo ikufaayo wakati inapotokea shida. Methali hii inalenga kuwatanabaisha watu kuwa binadamu anapopata shida ni watu walio karibu naye ndio watakaomsaidia.

A stick in the hand is the one that kills a snake.
  
13.Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno
Ganda la jana la muwa huwa limekauka, lakini chungu anapolipata huona ni mavuno maridhawa. Maana asiyezoea kuwa nacho, akipatapo hata kama ni kitu duni au hafifu namna gani na kidogo, hushangilia. Mathalani, kukengeuka kwa maadili kwa vijana barani Afrika na kuzamia tamaduni za kigeni.

The skin of yesterday’s sugar-cane is a whole harvest of an ant.

15.Gonga gogo usikie mlio wake
Ukitaka kujua mlio wa gogo, lipige na usikilize. Hili lina maana kuwa yakupasa kulichunguza jambo kwanza kabla ya kulihukumu (kulikabili).

Knock a log in order to hear the sound it makes.

16.Haba na haba hujaza kibaba 
Ukiweka akiba kidogo ya kitu kila mara, mwishoni utakuwa na akiba kubwa. Mwanzo wa makubwa ni madogo.

Little by little fills up the measure. (Little drops of water, little grains of sand, make a mighty ocean and a pleasant land).

17.Harakaharaka haina baraka
Jambo lifanywalo harakaharaka, haliwezi kufana. Mambo lazima yaende kwa kuzingatia mchakato wenye mpango na taratibu madhubuti.

Hurry, hurry, has no blessing. (More haste, less speed).

18.Iliyopita si ndwele, ganga ijayo
Mambo yaliyopita, yasishughulikiwe sana, bali tujizatiti kuyakabili na kuyadhibiti yale yajayo.

That which has passed is not a diease, cure what is coming.

19.Iwapo nia, njia hupatikana
Mtu anapofanya dhamira ya dhati ya kutaka kulitekeleza jambo, hawezi kukosa njia ya utekelezaji.

Where there’s a will, there’s a way.

20.Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza
Chochote usichokifahamu vizuri huwezi kukieleza kwa ufasaha.

A matter of which you are ignorant is like a dark night.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni