Viongozi wa chawakama tawi la mwalimu nyerere wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi prof H. Mwansoko wakati wa sherehe za uzinduzi wa chama hicho. kutoka kulia walio kaa ni rais mh Komanya wa pili ni makamu mkuu wa chuo mipango na fedha Dr Shawa wa tatu mgeni rasmi prof H. Mwansoko ambaye Mkurugenzi wa lugha katika wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo. 4 ni mwenyekiti ndugu Christopher Anthony. na mwisho ni mkuu wa idara ya elimu ndugu Msolwa
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LUMBA LUMBA KISWAHILI NA
UKUZWE UZALENDO+
1. CHAWAKAMA
mjibari, niwajuza haki yenu,
Natoa
langu shauri, hii ni dhamana yenu,
Moja
ilahi kahari, mmefanya Chama chenu,
Lumba lumba Kiswahili, Naukuzwe uzalendo.
2.
Msingoje kusubiri, kutendewa kazi zenu,
Msinune
mfikiri, fanyeni amuzi lenu,
Ni kama mwajiathiri, kuzuiwa kasi yenu,
Duri
Dawiri na Zari, tuwapambe CHAWAKAMA,
Lumba
lumba Kiswahili, naukuzwe uzalendo.
3.
Tumesimama majabari, kutongoa wito wetu,
Tunaifanya
dhamiri, yasambae mambo yetu,
Chuo
kiwe mshauri, kikiwa mlezi wetu,
Lumba lumba Kiswahili, na ukuzwe uzalendo.
4.
Na katu msijibari, Kiswahili lugha yetu,
Tamu isiyo shubiri, nzuri mno ya kikwetu,
Teo ifungwe tayari, kihodari kila utu,
Vigelegele na shangwe, Shangilia mashujaa.
5.
Mafunzo ya ikibari, yawe vitabuni
mwetu,
Mmeapa kwa hiari, kuikuza lugha yetu,
Yarabi na uibari, CHAWAKAMA ya wanetu,
Tawi limefunguliwa, CHAWAKAMA ya Nyerere.
6.
Hongereni mashujaa, kufungua tawi
lenu,
Akiba
ya manufaa, itunzeni amana yenu,
Sichoki
kuwa asaa, jahazi peleka kwenu,
Simameni
wahadhiri, shangilia mashujaa,
Lumba lumba Kiswahili, naukuzwe uzalendo.
7.
Mko wapi washairi, Malenga manguli wetu,
Tupokeeni mkiri, msitucheke
wenzetu,
Na hasa mtuamiri, hiki ni kiapo chetu,
Fenella
wa Mukangara, twaomba pongezi zetu.
8.
Natamatisha shairi, sina kinyongo na mtu,
Nimeeleza
dhahiri, Sijaficha hata kitu,
Kwa
kweli mko tayari, kulijenga bara letu,
Lumba lumba Kiswahili, naukuzwe uzalendo.
Mtunzi wa Shairi ni
Sikuzani wa Jalala (Nitendeje)
Limeruwazwa na
kughaniwa na Hajjat Shani Kitogo (Sauti
ya Asali)
Shairi
limeimbwa siku ya sherehe ya uzinduzi wa Tawi la Chama cha Wanafunzi wa
Kiswahili Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,
Tarehe 8/5/2015 katika Ukumbi wa Utamaduni.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni