Misamiati

Majina ya Ukoo
  1. Baba - mzazi wa kiume
  2. Mama - mzazi wa kike
  3. Dada - Ndugu wa kike (hutumika sanasana kurejelea ndugu wa kike mkubwa)
  4. Kaka - Ndugu mkubwa wa kiume.
  5. Babu – Baba wa babako au mamako
  6. Nyanya - Mamake mama au baba.
  7. Shangazi – ndugu wa kike wa Baba
  8. Mjomba – ndugu wa kiume wa mama
  9. Mpwa – mtoto wa nduguyo wa kike/kiume
  10. Umbu – jina wanaloitana ndugu wa kike na wa kiume
  11. Amu – ndugu wa kiume wa Baba
  12. Wifi – jina linalotumika baina ya mke na ndugu wa kike wa mume
  13. Mkaza mjomba – mke wa mjomba
  14. Binamu – mtoto wa shangazi/mjoma/amu
  15. Mkwe - mzazi wa mkeo.
  16. Mavyaa – mama mkwe
  17. Bavyaa – Baba mkwe
  18. Mkaza mwana – mke wa mwanao
  19. Mvyele – mzazi
  20. Mwana - mtoto wako (hasa wa kiume)
  21. Binti - mtoto wako wa kike
  22. Mjukuu - mtoto wa mwanao
  23. Kitukuu - mtoto wa mjukuu
  24. Kilembwe - mtoto wa kitukuu
  25. Kining’inia - mtoto wa kilembwe
  26. Shemeji - jina linalotumika baina ya mwanamke na ndugu za mumewe.


 Ulemavu
1.      Kiwete - asiyeweza kutembea wala kusimama  
2.      Kibongoyo - asiye na meno
3.      Kigugumizi - aliye na shida za kutamka maneno
4.      Bubu - asiyeweza kuongea
5.      Kiziwi - asiyeweza kusikia
6.      Kipofu – asiyeona
7.      Matege - mwenye miguu iliyopinda
8.      Chongo - mwenye jicho moja
Malipo
1.      Ada - malipo kwa mganga au ya hospitali
2.      Karo - malipo kwa ajili ya mafunzo (shuleni)
3.      Nauli - malipo ya kusafiri
4.      Kiingilio - malipo yanayotozwa watu ili kushiriki katika jambo Fulani
5.      Marupurupu - pesa za matumizi ya kila siku
6.      Ushuru - malipo kwa serikali
7.      Fidia - malipo kwa mtu baada ya kumkosea
8.      Kiinua mgongo - malipo anayotoa mtu kama shukrani kwa jambo alilotendewa au analotaka kutendewa
9.      Riba – malipo ya ziada yatokanayo na mkopo
10.  Mtaji – Kianzio katika bihashara inaweza kuwa pesa au rasilimali

11.  Kodi - malipo ya pango au uendeshaji wa biashara,bidhaa au kifaa
Kazi
1.dobihufanya kazi ya kuosha nguo
2.karanianayeangalia matumizi ya pesa katika benki au kampuni fulani
3.katibuanayeweka rekodi za mambo na orodha mbalimbali katika kampuni au idara fulani
4.kungwihufunza vijana jandoni
5.mchuhuzianayeuza bidhaa kutoka nyumba hadi nyumba
6.mfinyanzihufinyanga udongo kutengeza vyombo kama vyungu, n.k
7.mhandasianayefanya kazi ya kuunda au kurekebisha injini/mashine mbalimbali
8.mhasibumtu anayefanya kazi ya hesabu
9.mhunzihufua vyuma
10.mkatabianayeweka rekodi za vitabu katika maktaba, na kuwasaidia wanaotaka kuomba vitabu.
11.tabibuanayetibu watu 
12.topasikazi ya kuosha vyoo

Maoni 4 :