Jumanne, 9 Februari 2016

Mabadiliko ya Kileksia Katika Lugha ya Kiswahili

Utafiti Mdogo Kuhusu Mabadiliko ya Kileksia Katika Lugha ya Kiswahili.
(Grady ,1996) wanasema kuwa, kuna mabadiliko ya Kileksia ya aina mbili ambayo ni mabadiliko ingizi na mabadiliko potevu. Mabadiliko ingizi ni mabadiliko yanayotokana na ugunduzi wa teknolojia au maingiliano ya kiutamaduni, hali ambayo hupelekea mahitaji ambayo hutatuliwa kwa kuingiza maneno mapya. Hivyo, msamiati mpya huingizwa katika lugha kwa njia ya kuunda maneno mapya au kutohoa kutoka lugha nyingine. Kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili ipo misamiati iliyotoholewa kutoka lugha mbali mbali hasa lugha ya Kiingereza kama vile saikolojia, baiolojia, kompyuta, na treni.
 
Aina nyingine ya mabadiliko, kulingana na (O’ Grady na wenzake ,2006), ni mabadiliko potevu. Wataalamu hawa wanasema kuwa, haya ni mabadiliko ambapo matumizi ya neno fulani  hupotea baada ya kuingizwa kwa msamiati mpya. Kupotea kwa msamiati kunaweza kusababishwa  na mabadiliko ndani ya jamii hasa pale neno fulani linapoibuka na neno la zamani huachwa kutumiwa na hatimaye hupotea. Mfano, katika jamii ya Waswahili, msamiati bomani wenye maana ya ofisi ya mkuu wa wilaya uliokuwa ukitumika enzi za utawala wa Kijerumani umeacha kutumika kwa sasa ambapo  hutumika zaidi msamiati wa ofisi za mkuu wa wilaya.
 
(Holman ,2006) anasema kuwa, mabadiliko ya Kileksia ni mabadiliko ya kimsamiati. Anabainisha kuwa mabadiliko haya yapo ya aina mbili: mabadiliko ingizi na mabadiliko potevu. Mabadiliko potevu.  ni mabadiliko ambayo neno hupotea kabisa na neno jipya huibuka na kutumika badala ya neno la zamani. Mabadiliko ingizi, haya ni mabadiliko ambayo msamiati  huongezeka kwenye msamiati wa zamani. Hali hii husababishwa na kutohoa maneno kutoka lugha nyingine
.Kwa ujumla ni kwamba, mabadiliko ya Kileksia yanahusu mabadiliko ya kimsamiati ambapo msamiati fulani unaweza kupotea au ukaendelea kutumika sambamba na msamiati mpya ulioibuka.

Holman (2006), O’ Grady na wenzake (1996), kwa ujumla, wanabainisha kuwa, mabadiliko ya Kileksia ni mabadiliko yanayotokea kwa namna mbali mbali kama vile: mabadiliko yanayohusu kuingiza maneno mapya katika lugha na namna nyingine ni msamiati kupotea au kukosa matumizi.
 
Katika mabadiliko haya, uchambuzi wangu umeegemea namna tatu za utokeaji wa mabadiliko ya Kileksia katika lugha ya Kiswahili kama ifuatavvo:
(i)    Uingizaji wa Maneno Mapya katika Lugha.
Yapo maneno mapya ambayo yameingizwa katika lugha ya Kiswahili ambapo baadhi ya maneno hayo yana asili ya Kiswahili, mfano: Ngamizi. Pia, baadhi ya maneno yametoholewa kutoka katika lugha za kigeni kama vile Kiingereza, mfano neno: Digitari. Jedwali (2)  linabainisha maneno mapya ambayo yameingizwa katika lugha ya Kiswahi
Jedwali (2): Maneno Mapya Ambayo Yameingizwa katika Lugha ya Kiswahili
Msamiati
Maana
Bipu
Kitendo cha kupiga simu na kukata ghafla kabla haijapokelewa
Tovuti
Eneo katika mtandao wa kompyuta ambalo huelezea kuhusu shirika, mtu au taarifa fulani
Digitari
Mfumo wa kielektroniki unaotumia namba kusafirisha taarifa katika kompyuta
Vocha
Kadi inayohifadhi namba za muda wa maongezi ya simu
Kongoo
Kusanyo la maandishi mbali mbali
Maunzi Laini
Programu zinazowekwa katika kompyuta kwa ajili ya kuchakata taarifa
Ngamizi
Mashine inayotumika kurahisisha na kuchakata data
Uvinjari
Kitendo cha kutembelea katika mtandao wa intaneti
Puku
Kifaa kidogo chenye umbo la duara kinachoongoza mshale kwa ajili ya kutafutia sehemu au jambo fulani katika kompyuta
Maunzi ngumu
Vifaa vinavyounda kompyuta
Sakinisha
Kitendo cha kuingiza program katika kompyuta
Bonga
Kupiga simu
Umaizi bandia
Taaluma inayohusu mahusiano ya kompyuta na utambuzi wa binadamu
Chakata
Kutengeneza data ili ziwe katika namna inayoeleweka
Boda boda
Chombo chenye matairi mawili kinachoenda kwa kutumia mota( piki piki)
Utandawazi
Maingiliano ya kimataifa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia
TEHAMA
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Shuga mama
Mwanamke mwenye umri mkubwa mwenye mahusiano ya kimapenzi na vijana wenye umri mdogo
Shuga dadi
Mwanaume mwenye umri mkubwa mwenye mahusiano ya kimapenzi na wasichana wenye umri mdogo
Fataki
Mwanaume mwenye umri mkubwa mwenye mahusiano ya kimapenzi na wasichana wenye umri mdogo
Zatitisho
Namba zinazoruhusu kuingiza programu katika kompyuta
Nywila
Namba au herufi za siri zinazoruhusu kuingia katika mfumo fulani kikompyuta mfano kadi za kuchukulia hela benki au kwenye barua pepe
Oleza
Mwonekano w akitu katika kompyuta
Pakua
Kitendo cha kuchukua taarifa kutoka katika mtandao wa intaneti na kuiweka katika kompyuta
Bodidota
Kifaa katika kompyuta chenye namba, herufi na alama mbali mbali kinachotumika kuchapa maneno katika kompyuta
Fomati
Kufuta data zote katika kompyuta au kifaa cha kielektroniki
(ii)    Uingizaji wa Maneno Mapya lakini Maneno hayo Yanaendelea Kutumika Samba mba na Maneno ya Zamani.
Hii ina maana kwamba, maneno mapya hutumika sambamba na maneno ya zamani katika viwango sawa au viwango tofauti. Wakati mwingine maneno mapya yanapoingizwa katika lugha, yamekuwa hayapati nafasi kubwa ya kutumiwa na watumiaji wa lugha kutokana na sababu mbali mbali kama vile kuzoeleka kwa neno la kwanza. Kwa mfano, watumiaji wengi wa Kiswahili wamekuwa ni wagumu kutumia  neno lenye asili ya Kiswahili ngamizi na badala yake wameendelea kutumia neno Kompyuta lililotoholewa kutoka katika lugha ya Kiingereza. Hii imetokana na neno Kompyuta kuwa neno la kwanza kuibuka hivyo wazungumzaji wamelizoea tofauti na neno ngamizi na neno hili ngamizi limeendelea kutumiwa na baadhi ya watu hasa wanaisimu wa Kiswahili. Jedwali (3) linaonesha maneno ambayo yameingizwa lakini maneno hayo yanaendelea kutumika samba mba na maneno ya zamani
Jedwali (3): Maneno Mapya Ambayo Yameingizwa lakini Maneno Hayo Yanaendelea Kutumika Sambamba na Maneno ya Zamani.
Msamiati wa zamani
Msamiati mpya
Maana
Mudiri
Mkuu wa Idara
Mtu anayeongoza idara au ofisi fulani
Treni
Gari moshi
Gari linalotembea juu ya reli lenye mabehewa yaliyounganishwa
Onesha
onyesha
Kitendo cha kufanya jambo au kitu fulani kionekano
Kompyuta
Ngamizi
Mashine inayochakata na kurahisisha kazi
Mhujumu
fisadi
Mtu anayeiba rasilimali za nchi na kujilimbikizia mali
Imla
Dikteta
Kiongozi ambaye anatawala kwa mawazo na maamuzi yake mwenyewe
Televisheni
runinga
Chombo kinachopokea matangazo ya picha na sauti
Kabonimonoksaidi
Ukaa
Hewa chafu sana ambayo ni sumu kwa viumbe hai mfano: hewa inayotoka katika magari au viwanda
Halaiki
Kimbari
Kundi kubwa la watu wenye asili moja
Piki piki
Boda boda
Chombo kinachofanana na baiskeli kinachotumia injini ya mota
UKIMWI
umeme
Ugonjwa unaotokana na upunfufu wa kinga mwilini
Zaa
kujifungua
Kitendo cha mwanamke kutoa mtoto tumboni
bangi
ganja
Majani ya mmea wa kijani yenye kulevya
(iii)     Kupotea kwa Maneno.
Katika lugha ya Kiswahili, kuna baadhi ya maneno ambayo yalikuwa yakitumika zamani lakini kwa sasa maneno hayo hayatumiki. Baadhi ya maneno katika lugha ya Kiswahili yamepotea kutokana na sababu kama vile za kihistoria kwa mfano, neno ukabaila lilikuwa likitumika enzi za utawala wa kikoloni lakini baada ya kupata uhuru neno hilo limepotea au limeacha kutumiwa. Jedwali (4) linaonesha maneno ambayo yamepotea.
        Jedwali (4):  Maneno  Ambayo Yamepotea au Matumizi Yake Yamepungua
Msamiati
Maana yake
Ukabaila
Hali ya mtu kumiliki rasilimali nyingi ndani ya jamii na kuwapangisha au kuwatumikisha wengine mfano, kumiliki nyumba nyingi au ardhi. Mfumo huu wa uzalishaji ulitumika miaka ya zamani kabla ya kuja kwa wakoloni
Ngangari
Hali ya kuwa mbishi na kutoogopa jambo lolote
Ng’atuka
Kuondoka kwa hiyari katika nafasi ya uongozi. Neno hilo lilitumika katika enzi za ujamaa katika nchi ya Tanzania
Bwanyenye
Mtu mwenye mali nyingi na anayependa kustarehe bila kufanya kazi
Umwinyi
Hali ya kustarehe na kufanyiwa kazi.
Kachero
Askari kanzu au mtu anayechunguza habari za mtu au jambo kwa malengo fulani
paparazi
Mwandishi wa habari anayependa kuandika habari za siri za mtu mwingine bila ridhaa ya mhusika
Zeru zeru
Mtu mwenye ulemavu wa ngozi na nywele zake kuwa nyeupe
Kidosho
Msichana mzuri
Kiruka njia
Mwanamke asiyependa kukaa na mwanamme mmoja
Kisura
Mwanamke mrembo
Ujamaa
Kushirikiana kwa kila kitu katika maisha
Kuwadi
Mtu mwongo
liwali
Mtawala aliyechaguliwa na serikali anayeshughulikia mambo ya hukumu katika eneo alipo. Msamiati huu ulitumiwa enzi za ukoloni wa mjerumani
Akida
Msaidizi wa mkuu wa wilaya. Msamiati huu ulitumiwa enzi za ukoloni wa mjerumani
Midabwada
Nguo chakavu zilizochanika
maridadi
Mtu nadhifu
kapera
Mwanaume ambaye hajaoa
merikebu
Chombo cha kusafiria baharini kinachoendeshwa kwa mashine au upepo
sultani
Mtu mwenye cheo cha juu katika utawala wa kifalme. Msamiati huu ulitumiwa na waarabu walipokuwa wakitawala maeneo ya pwani
chakaramu
Mtu mtundu au mwenye wazimu
buriani
Hali ya kumuaga mtu
Utwana
Hali ya kutimikishwa na kufanyishwa kazi nyingi na kulipwa ujira mdogo au kutolipwa kabisa
Mwitu
Mkusanyiko wa miti mingi inayoleta giza ( misitu)
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni