Lugha yoyote iliyo hai hukua kwa kuongezeka maneno na msamiati.
Kiswahili kwa maneno haya matatu:
"Msadi' ni Kiswahili cha neno 'Consultant'.
"Kitamizi" ni kiswahili cha nano Incubator
"Makavazi ni Kiswahili cha neno Archives
Msamiati
|
Maana
|
Bipu
|
Kitendo cha kupiga simu na kukata
ghafla kabla haijapokelewa
|
Tovuti
|
Eneo katika mtandao wa kompyuta ambalo
huelezea kuhusu shirika, mtu au taarifa fulani
|
Digitari
|
Mfumo wa kielektroniki unaotumia
namba kusafirisha taarifa katika kompyuta
|
Vocha
|
Kadi inayohifadhi namba za muda
wa maongezi ya simu
|
Kongoo
|
Kusanyo la maandishi mbali mbali
|
Maunzi Laini
|
Programu zinazowekwa katika kompyuta kwa ajili ya kuchakata taarifa
|
Ngamizi
|
Mashine inayotumika kurahisisha
na kuchakata data
|
Uvinjari
|
Kitendo cha kutembelea katika
mtandao wa intaneti
|
Puku
|
Kifaa kidogo chenye umbo la duara
kinachoongoza mshale kwa ajili ya kutafutia sehemu au jambo fulani katika
kompyuta
|
Maunzi ngumu
|
Vifaa vinavyounda kompyuta
|
Sakinisha
|
Kitendo cha kuingiza program
katika kompyuta
|
Bonga
|
Kupiga simu
|
Umaizi bandia
|
Taaluma inayohusu mahusiano ya
kompyuta na utambuzi wa binadamu
|
Chakata
|
Kutengeneza data ili ziwe katika
namna inayoeleweka
|
Boda boda
|
Chombo chenye matairi mawili
kinachoenda kwa kutumia mota( piki piki)
|
Utandawazi
|
Maingiliano ya kimataifa kutokana
na maendeleo ya sayansi na teknolojia
|
TEHAMA
|
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
|
Shuga mama
|
Mwanamke mwenye umri mkubwa mwenye mahusiano ya kimapenzi na vijana wenye
umri mdogo
|
Shuga dadi
|
Mwanaume mwenye umri mkubwa mwenye mahusiano ya kimapenzi na wasichana
wenye umri mdogo
|
Fataki
|
Mwanaume mwenye umri mkubwa mwenye mahusiano ya kimapenzi na wasichana
wenye umri mdogo
|
Zatitisho
|
Namba zinazoruhusu kuingiza programu katika kompyuta
|
Nywila
|
Namba au herufi za siri zinazoruhusu kuingia katika mfumo fulani
kikompyuta mfano kadi za kuchukulia hela benki au kwenye barua pepe
|
Oleza
|
Mwonekano w akitu katika kompyuta
|
Pakua
|
Kitendo cha kuchukua taarifa kutoka katika mtandao wa intaneti na kuiweka
katika kompyuta
|
Bodidota
|
Kifaa katika kompyuta chenye namba, herufi na alama mbali mbali
kinachotumika kuchapa maneno katika kompyuta
|
Fomati
|
Kufuta data zote katika kompyuta au kifaa cha kielektroniki
|
Msamiati wa zamani
|
Msamiati mpya
|
Maana
|
Mudiri
|
Mkuu wa Idara
|
Mtu anayeongoza idara au ofisi fulani
|
Treni
|
Gari moshi
|
Gari linalotembea juu ya reli lenye mabehewa yaliyounganishwa
|
Onesha
|
onyesha
|
Kitendo cha kufanya jambo au kitu fulani kionekano
|
Kompyuta
|
Ngamizi
|
Mashine inayochakata na kurahisisha kazi
|
Mhujumu
|
fisadi
|
Mtu anayeiba rasilimali za nchi na kujilimbikizia mali
|
Imla
|
Dikteta
|
Kiongozi ambaye anatawala kwa mawazo na maamuzi yake mwenyewe
|
Televisheni
|
runinga
|
Chombo kinachopokea matangazo ya picha na sauti
|
Kabonimonoksaidi
|
Ukaa
|
Hewa chafu sana ambayo ni sumu kwa viumbe hai mfano: hewa inayotoka
katika magari au viwanda
|
Halaiki
|
Kimbari
|
Kundi kubwa la watu wenye asili moja
|
Piki piki
|
Boda boda
|
Chombo kinachofanana na baiskeli kinachotumia injini ya mota
|
UKIMWI
|
umeme
|
Ugonjwa unaotokana na upunfufu wa kinga mwilini
|
Zaa
|
kujifungua
|
Kitendo cha mwanamke kutoa mtoto
tumboni
|
bangi
|
ganja
|
Majani ya mmea wa kijani yenye
kulevya
|
Msamiati
|
Maana yake
|
Ukabaila
|
Hali ya mtu kumiliki rasilimali nyingi ndani ya jamii na kuwapangisha au
kuwatumikisha wengine mfano, kumiliki nyumba nyingi au ardhi. Mfumo huu wa
uzalishaji ulitumika miaka ya zamani kabla ya kuja kwa wakoloni
|
Ngangari
|
Hali ya kuwa mbishi na kutoogopa jambo lolote
|
Ng’atuka
|
Kuondoka kwa hiyari katika nafasi ya uongozi. Neno hilo lilitumika katika
enzi za ujamaa katika nchi ya Tanzania
|
Bwanyenye
|
Mtu mwenye mali nyingi na anayependa kustarehe bila kufanya kazi
|
Umwinyi
|
Hali ya kustarehe na kufanyiwa
kazi.
|
Kachero
|
Askari kanzu au mtu anayechunguza
habari za mtu au jambo kwa malengo fulani
|
paparazi
|
Mwandishi wa habari anayependa
kuandika habari za siri za mtu mwingine bila ridhaa ya mhusika
|
Zeru zeru
|
Mtu mwenye ulemavu wa ngozi na
nywele zake kuwa nyeupe
|
Kidosho
|
Msichana mzuri
|
Kiruka njia
|
Mwanamke asiyependa kukaa na
mwanamme mmoja
|
Kisura
|
Mwanamke mrembo
|
Ujamaa
|
Kushirikiana kwa kila kitu katika
maisha
|
Kuwadi
|
Mtu mwongo
|
liwali
|
Mtawala aliyechaguliwa na
serikali anayeshughulikia mambo ya hukumu katika eneo alipo. Msamiati huu
ulitumiwa enzi za ukoloni wa mjerumani
|
Akida
|
Msaidizi wa mkuu wa wilaya.
Msamiati huu ulitumiwa enzi za ukoloni wa mjerumani
|
Midabwada
|
Nguo chakavu zilizochanika
|
maridadi
|
Mtu nadhifu
|
kapera
|
Mwanaume ambaye hajaoa
|
merikebu
|
Chombo cha kusafiria baharini kinachoendeshwa kwa mashine au upepo
|
sultani
|
Mtu mwenye cheo cha juu katika utawala wa kifalme. Msamiati huu ulitumiwa
na waarabu walipokuwa wakitawala maeneo ya pwani
|
chakaramu
|
Mtu mtundu au mwenye wazimu
|
buriani
|
Hali ya kumuaga mtu
|
Utwana
|
Hali ya kutimikishwa na kufanyishwa kazi nyingi na kulipwa ujira mdogo au
kutolipwa kabisa
|
Mwitu
|
Mkusanyiko wa miti mingi
inayoleta giza ( misitu)
|