DONDOO KUHUSU
UHUSIANO BAINA YA LUGHA NA JAMII@
Okoa Simile
a . Lugha ni nini?
Lugha - ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokubaliwa na
watu au jamii ili zitumike katika mawasiliano yao ya kilasiku ili kueleza
hisia, mawazo, matakwa na mahitaji yao.
b . Jamii ni nini?
Jamii
- ni kundi la watu wanaoishi katika eneo Fulani, wanao
jitambulisha kama kundi moja, wenye utamaduni mmojana na lugha moja.
c . Isimu jamii ni nini?
Isimu Jamii - ni tawi la isimu
(elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na
uhusiano baina yake. Tawi hili huzingatia matumizi ya lugha katika mazingira
tofauti; aina mbali mbali za lugha na mazingira yake; uhusiano kati ya lugha na
utamaduni wa jamii inayoitumia.
King’ei (2010), anaeleza kuwa,
kwanza lugha ni zao la jamii, na ni kipengele muhimu sana cha utamaduni wa
jamii husika. Pili, lugha hutumiwa na jamii kuhifadhi amali na utamaduni wake
na hasa kama chombo maalumu cha kuwezesha wanajamii kuwasiliana. Hivyo isimu
jamii hueleza na kufafanua mahusiano ya karibu kati ya lugha na jamii ambayo
ndiyo mama wa lugha
.
.
d . Uhusiano huu baina ya lugha na
jamii.
i.
Lugha
ni zao la jamii, ni sehemu ya jamii kwani ni sehemu ya utamaduni wa jamii
husika. Lugha ni njia inayotumiwa na wanajamii ili kueleza na kusambaza
utamaduni wake.
ii.
Mwanaisimu
Sapir na Whorf, wanaeleza kuwa lugha huathiri sana na kudhibiti jinsi wazungumzaji na watumiaji wa lugha wa jamii fulani wanavyoufasili ulimwengu
wao. Kulingana na wanaisimu hawa muundo wa maana katika lugha ndiyo msingi wa
mawazo au utaratibu wa fikra. Mwanadamu hawezi kufikiri kamwe bila kutumia
lugha. Jambo hili linamaanisha kuwa kwa vile mawazo na fikra za mwanadamu vinaukiliwa
na lugha basi inawezekana kudhibiti
fikra za wanajamii kwa kuidhibiti lugha yao. Katika muktadha ya Kitanzania nan
chi nyingi za Kiafrika , hili limthibitika kwani, miongoni mwa Watanzania walio
wengi wanahusisha maarifa na lugha fulani (mathalani kiingereza). Hii inatokana
na imani iliyopandikizwa na wakoloni kwamba lugha ya Kiingereza ni lugha ya
utaarabu na lugha ya kitaaluma. Hivyo uwezo wao wa kudhibiti matumizi ya lugha
kwa kututoa katika matumizi ya lugha mama yamefanikisha kuelekeza fikra za wanajamii
hawa kwenye mawazo kwamba taaluma na usomi ni kujua Kiingereza.
iii.
Kwa
mujibu wa King’ei (2010) lugha hulejelea mazingira ya jamii husika, na ndiyo
maana watu wenye lugha sawa na wanaishi katika mazingira tofauti wanaweza kuwa
na mtazamo tofauti ya kimaisha na ufasili wao wa ulimwengu
iv. Kwa kutumia nadharia ya ‘ukiliaji wa kiisimu’ (Linguistic Determinism) lugha ndiyo inayoongoza mawazo ya watu na huathiri hata maana ambazo watu wanazitoa kuelezea dhana na mitazamo fulani katika lugha zao.
iv. Kwa kutumia nadharia ya ‘ukiliaji wa kiisimu’ (Linguistic Determinism) lugha ndiyo inayoongoza mawazo ya watu na huathiri hata maana ambazo watu wanazitoa kuelezea dhana na mitazamo fulani katika lugha zao.
v.
Kwa
njia ya lugha watu wa jamii Fulani wanapata nafasi ya kujadili masuala mbali
mbali yanayohusu maendeleo ya jamii.
vi.
Kama
hiyo haitoshi, Austin (1962) anasema kuwa, ni muhimu kuhusisha matumizi ya
lugha na muktadha wake wa kijamii kwani
lugha huwa na matumizi tofauti kama kutoa mapendekezo, kuahidi, kukaribisha,
kuomba, kuonya, kufahamisha, kuagiza, kukashifukusifu, na kuapiza.
vii.
Lugha
ndicho chombo kinachotumika kuwaleta pamoja na kuwaunganisha wanajamii hukuikisaidia kuimarisha uhusiano miongoni mwa wanajamii. Katika muktadha wa
Kiafrika, kwa mfano, heshima ya mtu inatambulishwa na jamii ya watu ndiyo maana
waswahili wana msemo unaosema “mtu ni
watu”. Kauli hii kwa ujumla inatuonesha kuwa katika harakati za maisha za
wanajamii heshima na kukubalika kwa mtu pamoja na kueleweka kwake kunatokana na
namna mtu anavyohusiana na wanajamii wengine pamoja na mambo mengine ikiwa ni
kutumia lugha kwa ufasaha. Haya yote yanawasilishwa kutoka katika jamii moja
kwenda katika jamii nyingine kwa kutumia lugha ambacho ndicho chombo muhimu cha
mawasiliano.
viii.
Jamii
hutambulika kwa kutumia lugha. Lugha huwa na uwezo wa kuonesha sifa fulani
kuhusu mzungumzaji, anayerejelewa na uhusiano uliopo kati ya wanajamii.
Utamaduni hutambulishwa katika maeneo mbali mbali ya ulimwengu kwa kutumia lugha
pia. Kwa mfano, katika fasihi ya kabila la Wahaya, tunatambua mambo mbali mbali
yanayohusu kabila hili hasa katika kipengele cha majigambo kutokana na namna
wanajamii hawa wanavyotumia lugha yao kujipambanua kwa jamii nyingine.
ix.
Lugha
pia hutumika katika kurithisha mila na desturi za jamii ikiwa na pamoja na
kutolea elimu. Binadamu huweza kufunzwa na kupewa maadili mbali mbali kwa
kutumia lugha ili waweze kujitambua kuwa wao ni akina nani na wapo ulimwenguni
kwa malengo gani. Kwa mfano, watoto huwezwa kufunzwa masuala yanayohusu uana wao
ambao hutokana na jinsia yao. Kwa
kutumia lugha. Pamoja na kuwa wanajamii wanaona matendi yanayotendwa na jamii
nyingine au ndani ya jamii hiyo lakini wanahitaji namna ya kuambiwa juu ya
uzuri au ubaya wamatendo hayo, kufuata au kuto yafuata. Hapa lugha inachukua
nafasi yake.
Marejeo
King’ei,
K. (2010). Misingi ya Isimu Jamii.
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tanzania.
Austin, J.L. (1962). How to do things with Words. Oxford.
Oxford University Press.